Tangu nimjue Yesu
Tangu nimjue Yesu na kumkaribisha moyoni mwangu
Yalopita yamepita na kuvaa utu upya ndani yangu
Sijitaabishi tena ya kale hayana nafasi kwangu
Nime vikwa utu upya, nimekuwa kiumbe ndani ya Yesu x 2
Utu wangu wa zamani umezikwa na kuvaa utu upya
Sikumbuki ya zamani, Yesu yu ndani yangu
Nachuchumilia taji kwa sasa yalopita yamepita
Dunia kwa heri, yalo pita yamepita. x2
Maisha ndani ya Yesu ni raha isiyo kuwa kifani
Mazito hurahisishwa yatoweka kwa jinsi usivyojua
Mambo yote ya zamani, hayakumbukwi tena maishani
Mpe Yesu moyo wako, utaona yote yana wezekana