TAZAMA
1. Tazama damu uliyoimwaga msalabani
Ili dhambi zangu mimi nitakaswe
(Niokolewe nisiende jehenamu ×2)2
:/: Mate ulitemewa
Ulinyamaza kimya
Mkuki ulichomwa
Ulinyamaza kimya
Tena kudhalilishwa
Ulinyamaza kimya
(Yote haya ulitendewa
Ili mimi niokolewe ×2)
2. Tazama pazia lile la hekalu lilipasuka
Niweze kutubu makosa kwa Yesu
(Nisamehewe na wokovu niupate x2) x2
3. Ee ndugu kumbuka kifo cha Yesu msalabani
Alivyoteseka ili uokoke
(Utubu leo ukaache dhambi zako x2) ×2