TAZAMA LIPO ANGAMIZO
1. Tazama liko angamizo, kwayo mataifa yote,
ijapopigwa tarumbeta, kuwaonya waache,
uovu wao wakakaidi, wakafa wasiponywe nafsi,
damu za watu kaidi zitakua juu ya nafsi zao wenyewe.
Mungu kaweka mamlaka na uweza kinywani mwako,
uwape maonyo haya sema nao,
tazama usipowaonya wakafa katika uovu,
damu yao itadaiwa mikononi mwako. X2
Chorus:
Basi wewe mwanadamu nimekuweka, kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli.
(Lisikie), lisikie neno hili (Neno hili) kinywani mwangu ukawape,
maonyo yangu watu wapate kupona X2
2. Baba Mungu hapendezwi na dhambi, za wanadamu,
hapendi hata mmoja afie dhambini, aghairi atubu na kuacha,
hizo njia hizo zake mbaya hatokufa ataishi,
sema nao usinyamaze usijepata angamia.