WImbo: Timotheo
Waimbaji: Kwaya Ya Uinjilisti Kijitonyama
Album:Dunia
Mtunzi:
Ukisoma Timotheo wa kwanza sura ya nne,
msitari ni ule wa kumbi na mbili wahusu Vijana x2
Solo: Mahusia ya Paulo kwa timotheo hata na sisi, hebu soma ufikiri vile ambavyo anatuambia
Mtu yoyote asiudharau ujana wako kijana,
bali uwe kielelezo kwao wote wamwaminio Bwana
Katika usemi, mwenendo, upendo, ooh imani usafi, ee ndugu
Mtu awaye yote asiudharau ujana wako kijana,
bali uwe kielelezo kwao wote wamwaminio Bwana
Uyatafakari hayo mahusia ya Paulo,
ni mwongozo wa maisha yaliyomema yakufurahisha x2
Solo: Kaa chini uchunguze vile ambavyo anatuambia, kwani ni ya busara na ya hekima utafaidika.
Jirekebishe kijana kwa mahusia ya Paulo
ni muongozo wa maisha yaliyo mema ya kufurahisha. x2
Solo: Ukiyazingatia mbele za watu utawapendeza wao wakuonao pia na wale wakusikiao