Wimbo: TOKEA ZAMA
Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama
Album: Yatafakarini
Mtunzi:
Tokea zama za mababu zetu, walimtolea Bwana mavuno x2
Leta, leta, leta mavuno kwa Bwana x2
(Wewe wajua) wewe wajua ulipanda wapi
Hivyo Bwana ataka mavuno x2
Watu wengi wanaulizana, mavuno maana yake nini
Watu wengi wanasemezana eti mavuno mradi wa kanisa
Kumbe wana, wanajidanganya, mavuno ni Mungu kasema
Ukisoma kitabu cha malaki wa tatu, saba kuendelea
Bwana asema ninyi mwaniibia, zaka pia na ile dhabihu
Mmeficha vile vilivyo vingi, vichache mmeleta kwangu
Leteni zaka iliyo kamili, na Bwana atawabariki
Leta, leta, leta mavuno kwa Bwana x2
(Wewe wajua) wewe wajua ulipanda wapi
Hivyo Bwana ataka mavuno x2
Ukisoma kitabu cha matendo wa tano mstari wa kwanza
Utaona Anania na Safira walificha mavuno kwa Bwana
Na tazama waliangamizwa wakafa wote kwa dhambi hiyo
Leta, leta, leta mavuno kwa Bwana x2
(Wewe wajua) wewe wajua ulipanda wapi
Hivyo Bwana ataka mavuno x2