Phesto

TONE LA DAMU

May 21, 2025

WIMBO: TONE LA DAMU
Kwaya Ya Uinjilisti KIJITONYAMA
Mtunzi: Dkt Tuntufye Mwakisisile

Tone la damu yako Yesu la thamani ee
Msalabani ulitoa tone hilo
Tone la damu lililotoka ktk ubavu wako
Tone la damu lililochuruzika kichwani pako

Lidondokee machoni (machoni)
Niweze kukuona (kukuona)
Lidondokee sikioni (sikioni)
Niweze kusikia (sauti yako oh)
Naomba tone la damu yako Yesu

W-Naomba tone la damu ya Yesu
S- Mimi siombi pipa la damu, naomba tone tu
W-Naomba tone la damu ya Yesu
S-Tone linatosha sana baba kuniosha dhambi mimi
W-Naomba tone la damu ya Yesu
S-Tone hilo la mwanakondoo

Tone hilo la simba wa Yuda
Tone hilo la mwanaume Yesu

W-Eee tone lina uponyaji aaah
Tone limejaa amani eee
Tone lina matumaini

III-Ukipata shida ndugu kimbilia tone ee
W-Kimbilia tone la damu yake Yesu mwokozi
S-Majaribu yakikusonga ukaoge tone eh
W-Ukaoge tone la damu yake Yesu mwokozi
S-Tone hilo×2 oh
W-Tone lauhisha linaponya
Linatakasa aah eeeh
Amini tone la damu
Oh eee Tone la damu ya Yesu

2. S-Yule tajiri aliomba tone la maji
Liburudishe ulimi akate kiu
Je tone lako lililochuruzika kwa mijeledi
Tone la damu lililo huruzika kwa misumari
S-Lidondokee kinywani
Niweze kukunena
Lidondokee rohoni-rohoni
S-Niweze kutakaswa dhambi zangu ohh

Article by Phesto

Lorem ipsum amet elit morbi dolor tortor. Vivamus eget mollis nostra ullam corper. Natoque tellus semper taciti nostra primis lectus donec tortor fusce morbi risus curae. Semper pharetra montes habitant congue integer nisi.

Leave a Comment