TUKIYASOMA MAANDIKO
1.S: Tukiyasoma maandiko ooh ya kale yale yaliyotabiriwa na manabii
Nabii Isaya alitabiri na Yohana mbatizaji naye hivyo hivyo, atazaliwa Masiya katika hali ya umasikini, (Kazaliwa kwa taabu kafundisha kwa taabu Yesu kisha walimtesa na kumuua Golgata) x2
2. S: Walidhani ndio mwisho wake Bwana Yesu walipomsulubisha pale msalabani
Kina mama watatu walishangaa walipoona lile jiwe limeondolewa walisahau ya kwamba hakika Yesu yeye alisema
(ilimpasa kufa siku ya tatu kufufuka yeye simba wa Yuda na Leo hii yuko hai) x2
3. S: Yesu ni yeye yule jana Leo hata milele, ukimpokea yeye utayashinda yote
Damu yake ya thamani ilimwagika kutuosha dhambi zetu sisi wanadamu kutupatanisha Yesu na Baba Mungu wetu wa mbinguni ndugu tumpokee tufanyike wana wa Mungu ili kibali tupate na mbinguni tuingie x2
CHORUS :
Amefufuka Leo amefufuka
Yesu ameshinda mauti amefufuka
S: Haya twendeni
W: Haya twendeni jama haya twendeni tukalione kaburi lake liwazi.