Tunakushukuru
Tunakushukuru eMungu wetu Mtakatifu
Kutuvusha salama tena mwaka uliopita
Umetukinga na hatari nyingi twakushukuru
Hakuna wa huruma kama wewe Mungu wetu x2
Katika shida….
Ulitukinga, ooh ulitukinga Bwana uhimidiwe
Kwenye hatari…
Ulitukinga, ooh ulitukinga Bwana uhimidiwe
….
Wengi miongoni mwa ndugu zetu walitutoka,
Tukawa katika majonzi mengi siku hizo
Faraja yako ilitupa nguvu tukasimama
Tumekwisha kuyasahau yote twasonga mbele x2
Sisi tumebaki salama baba kwa neema yako
Uovu mwingi mbele yako sisi tuliutenda
Utujalie mwaka huu sisi tukupendeze
Na mibaraka yako Mungu usitunyime