Ufalme wa Mbinguni
Ufalme wa mbinguni, umefanana
Na hazina iliyositirika katika shamba
Mtu alipoina aliificha, akauza vyote alivyonavyo kainunua x2
Ufalme wa Mbinguni kwetu sisi kitu cha thamani
Hivyo ndugu mpendwa, jitahidi kuingia kule
Achana na vyote vya dunia hii
Vyakupoteza, amini Bwana Yesu, uingie uzimani x2
Ufalme wa mbinguni umefanana
Na mfanyabiashara mwenye kutafuta lulu nzuri
Naye alipoiona yenye thamani, aliuza vyote alivyo navyo kainunua x2