ULIMI KIUNGO KIDOGO
1. Ulimi kiungo kidogo chaweza kuleta majuto chaweza kuleta machungu na kuleta mafarakano tafakari uyanenayo chunga Sana ulimi wako uwe mwaminifu kwa wote wakati wote
Chorus: unahangaika bure chunga ulimi wako ndugu epuka Mambo mabaya kinywani mwako ulimi waleta machungu kwa kuyanena Mambo mabaya ulimi waleta huzuni waleta majuto mwisho ni kilio
2 Ni Kama Moto masituni uwakavyo bila huruma chanzo chake Ni kiberiti kiberiti kidogo sana Mwisho wake unaenea na kuleta maangamizo chunga Sana ulimi wako wakati wote
Mwl KIBASO