ULIMI WAKO UTAKUPONZA
1.Ulimi wako utakuponza, ni kiungo kidogo kwako eeh mwanadamu.
Ni kiungo hatari kukuangamiza, kinaleta furaha, kinaleta huzuni.
Ulimi wako ndugu wautumiaje x2
2. Bwana ninakuomba funga ulimi wangu.
Niweze kuyanena ya kupendezayo
Natamani kunena mambo yaliyo mema ila ulimi wangu ndio unaniponza x2
CHORUS:
Ulimi wako wautumiaje, ulimi wako wanena vipi
Ni ulimi wako utakuponza
Ni ulimi wako waweza kukuponya.