Unajielewa Wazi
Unajielewa wazi wamkosea Mungu
Muumbaji wako aliye kuumba wewe
Maovu yamekuzidi umrudie Yesu
Bwana wako mwokozi wetu x2
Twaitazamia Nuru
Nuru na kumbe tunakwenda gizani
Twautazamia mwanga,
Mwanga na kumbe giza linatokea x2
(Ondoka) Ondoka na uangaze, (Nuru yako) Nuru yako imekuja
(Na utukufu) Na utukufu wa Bwana (Yesu) umeshakushukia we
Moyo wako ugeuze umtazame Bwana
Umtumainie maishani mwako wewe
Hakuna mwingine tena ila ni Yesu Bwana
Bwana wako mwokozi Yesu x2
Uwe na umoja nasi tusemezane sasa
Katika jina lake Bwana wetu muumbaji
Dhambi zetu zisafishwe tutakasike wote
Haleluja mwokozi wetu