*KARIBU*
Wapendwa,
Karibuni kwenye Kundi hili la waimbaji ambao wamewahi kuhudumu katika kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama.
Shalom kaka na dada zangu tumeona tuwe na group la waimbaji wa zamani ili *tusipoteze kumbukumbu ya utumishi huu.* Hasa kwa wale ambao kwa sababu mbalimbali za kimaisha na kimazingira hawana nafasi/uwezo wa kuhudumu na kwaya kwa sasa.
*Ni matuamini kwamba Kundi hili litaendelea kuleta umoja wa kipendwa,* na kudumisha udugu na upendo ambao umekuwa ukipokezwa vizazi na vizazi kuanzia uasisi wa kwaya yetu mpaka sasa, na hata mbeleni.
*Hivyo kila mmoja wetu, kwa nafasi yake atumike kuwa baraka kwa mwingine, na kwa kwaya yetu pia.*
Mungu ana njia nyingi, inawezekana sana pia kupitia kundi hili, mmoja wetu akapata wito na mshawasha wa kurudi tena hudumani, ama kuhusika na huduma kwa mfumo tofauti. Maana shambani mwa Bwana kazi nyingi.
*_Usiposhika kipaza sauti, basi unaweza kuwezesha kipaza sauti, na mwingine anaweza kuombea huduma._*
*Karibuni na Mungu atubariki sote.*