Phesto

USIOGOPE

May 21, 2025

USIOGOPE

Chorus: Usiogope eeh ndugu, Yesu yupo mbele yako, yupo nyuma yako, kushoto kulia Yesu yupo, zaidi akufunika kwa Damu yake ya thamani, usiogope ee

Verse 1
Kamwe usije ukawaza Mungu kakuacha ee ndugu, ujapopitia majaribu mbalimbali eeh,
Mungu amekusudia kukutengenezea njia, ukishayashinda yote imani yako itakua,
kumbuka majaribu kipimo cha imani yako, usiogope..

Chorus

Verse 2.
Hata kama nyuma yako kwaja majeshi ya farao,
hata kama mbele yako kunayo bahari ya shamu,
hofu na mashaka visiutawale moyo wako e ndugu mpendwa,
maana kwa neno lake Bwana bahari itakuwa njia,
maana kwa neno lake Bwana bahari itakuwa njia

Chorus

Verse 3

Solo: Subiri yeyeye subiri kutoka kwa Yesu, subiri yeyeye, atakujibu kwa wakati, subiri yeyeye majibu kutoka kwa Yesu subiri yeyeye, utajibiwa kwa wakati eeeh

Wote: Subiri yeyeye, subiri kutoka kwa Yesu, subiri yeyeye atakujibu kwa wakati

Solo: …..free style
Wote:Subiri yeyeye, subiri kutoka kwa Yesu, subiri yeyeye atakujibu kwa wakati

Verse 4:
Yeye ni mwanzo na tena ni mwisho ahadi zake hazipimwi kwa muda,
miaka elfu kwenye hii dunia kwake Bwana sawa na siku moja X2
subiri eeh, subiri eeh, subiri eeh baba, subiri eeh, subiri eeh,
subiri eeh mama, subiri eeh, subiri eeh, subiri eeh kaka, subiri eh subiri eeh,, leleleleee

Wote: Subiri yeyeye, subiri kutoka kwa Yesu, subiri yeyeye atakujibu kwa wakati

Article by Phesto

Lorem ipsum amet elit morbi dolor tortor. Vivamus eget mollis nostra ullam corper. Natoque tellus semper taciti nostra primis lectus donec tortor fusce morbi risus curae. Semper pharetra montes habitant congue integer nisi.

Leave a Comment