VIREJESHWE
1. Virejeshwe,virejeshwe,
Bwana naomba virejeshwe x2
Hamu ya kukupenda wewe,na pia kukutumikia
Bwana naomba virejeshwe
Nia ya kuwasaidia, wale walio wahitaji
Bwana naomba virejeshwe x2
Virejeshwe…..x2
2. Afya yangu iliibiwa,na Uchumi uliibiwa
Bwana naomba urejeshwe
Ukoo umesambaratika,watoto hawaeleweki
Bwana naomba warejeshwe x2
Warejeshwe, warejeshwe
Bwana naomba warejeshwe x2
3. Yaliyoliwa na nzige,yaliyoliwa na parale
Bwana naomba yarejeshwe
Yaliyoliwa na madumadu,yaliyoliwa na tunutu
Bwana naomba yarejeshwe x2
Yarejeshwe ,yarejeshwe x2
Bwana naomba yarejeshwe x2
Virejeshwe,virejeshwe x2
Bwana naomba virejeshwe x2