WAHUBIRI
Wahubiri, msipoisema kweli watahukumi kwa kazi mbaya
Wamekuwa wamshahara tu, na Bwana asema Ole kwa watumishi hao
Na wakristo tusipo mkiri Yesu kwamba ni Mwokozi wetu tutahukumiwa
Ole wetu tukijifariji kwamba hakuna wokovu kweli tutahukumiwa
(Bwana Yesu) Bwana Yesu ametoa tangazo dunia nzima wote wanalisoma
(Tena aita) Anaita njooni msumbukao na dhambi zenu nitawapumzisha
(Ni wakati) Ni wakati wako sasa kutubu uende kwa Yesu upate pumziko
Na wasomi msipo okoka leo, mtahukumi kwa kiburi chenu
Matajari msipo okoka leo, mtahukumiwa kwa kiburi chenu
Akina baba msipo okoka leo, mtahukumiwa kwa kiburi chenu
Akina mama msipo okoka leo, mtahukumiwa kwa kiburi chenu
Tazameni, siku zinakwisha ndugu, ishara nyingi sana tumeshaziona
Tukumbuke dunia si yetu hii, twapunga upepo hapa kisha twaondoka
Kisha wote tutakunika kwake, mbele ya Mungu wetu aliye tuumba
Tutalipwa sawa na matendo yetu kama ni uzima au kwenda jehanamiu