YATAFAKARINI
Yatafakini maneno ya Bwana kwa kinywa cha Hagai akisema
Nyumba zenu ni nzuri, zimejengwa kwa mbao
Lakini nyumba yangu mwaiacha yaharibika x2
Panda milimani, lete miti ya kutosha
Lete na sadaka yako, tuijenge nyumba ya Bwana
Lete na mavuno nayo mtolee Bwana
Toa nawe ufurahi, tuijenge nyumba ya Bwana x2
Kanisa la Bwana, leo lahitaji
Liejengwe na wakirsto lipendeze
Ni nyumba yake Mungu hapo twakutanika
Na kuzungumza na Baba Yetu wa Mbinguni x2
Mbingu na dunia ni mali ya Bwana, fedha ulizonazo mali yake
Uzilete kwa Bwana, zijenge nyumba yake
Azungumze nasi kama baba na watoto x2